Selena Gomez na mpenzi wake Benny Blanco kuachia album mpya.
Joyce Shedrack
March 20, 2025
Share :
Selena Gomez ambae ni mwanamuziki na mfanyabiashara pamoja na mpenzi wake Benny Blanco ambae ni Producer wa muziki wamepanga kuachia Album yao ya 'I SAID I LOVE YOU FIRST" usiku wa kuamkia machi 21 baada ya kuachia wimbo wao wa pamoja #Scared of Loving You mwanzoni mwa mwezi march.
Album hiyo ambayo itaenda sambamba na mipango ya Harusi yao baada ya kuvishana Pete ya uchumba mwishoni mwa 2024, inakuwa ni Moja kati ya Album ambazo Gomez amedai kuwa imemfanya Kutumia muda mwingi na kutumia Mapenzi yake yote ya Kimuziki kwenye kuandaa Album hiyo.
Album ya mwisho ya #SelenaGomez ilikuwa ni #Rare aliyoitoa miaka mitano iliyopita akiwa bado hajaanza mahusiano ya kimapenzi na mpenzi wake #BennyBlanco ambae ni ‘producer’.