Senegal haina uwanja wa timu ya taifa kucheza mechi za CAF
Sisti Herman
September 11, 2026
Share :

Kuelekea mchezo wa kuwania kufuzu AFCON 2027 kati ya Senegal na Msumbiji, Mashabiki wa Senegal wamelalamika wakishutumu kwanini mechi hiyo isichezwe Dakar, nyumbani kwa Senegal.
Hakuna uwanja nchini Senegal wenye vigezo vya mchezo huo kuchezwa unaopatikana kwa sasa. Uwanja wa Abdoulaye Wade hautumiki kutokana na maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Vijana ya Dakar 2026, huku viwanja vingine nchini humo vikielezwa kutokuwa katika hali nzuri.
Mechi hiyo ya mchujo wa AFCON 2027 sasa itachezwa jijini Maputo, Msumbiji, tarehe 25 Septemba.





