Senegal inpitia kipindi kigumu kisa ukata wa fedha.
Joyce Shedrack
June 22, 2026
Share :
Timu ya taifa ya Senegal inapitia kipindi kigumu nje ya uwanja huku wakiwa kwenye michuano ya Kombe la Dunia ripoti zinaeleza kuwa nyota hao bado wanadai bonasi zao.

• Wachezaji bado hawajalipwa fedha zao za zawadi walizoahidiwa baada ya kushinda Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) na kufuzu kwa Kombe la Dunia.
• Kuna malalamiko kuhusu ubora duni wa hoteli iliyowekewa timu kwa ajili ya kambi yao ya mazoezi nchini Marekani.
• Pia hawakuambatana na mpishi mkuu wa timu kutokana na “bajeti ndogo” iliyotengwa na Shirikisho la Soka.
• Hali hiyo imewalazimu wachezaji kuagiza chakula chao wenyewe ili kuhakikisha wanakula vyakula vya afya.
• Kocha mkuu, Pape Thiaw, anaendelea kufanya kazi hadi leo bila mkataba rasmi na bado anadaiwa mshahara wa miezi sita.





