Senegal kuisaidia Mali katika vita dhidi ya makundi ya wanajihadi
Eric Buyanza
July 29, 2026
Share :

Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, amesema nchi yake inaiunga mkono Mali kwa asilimia 100, akisema yuko tayari kuisaidia nchi hiyo ya Jirani katika vita dhidi ya wanajihadi wa kiislamu, matamshi aliyoyatoa wakati wa ziara yake mjini Bamako Jumanne Julai 2026.
Faye amezuru Mali kwa mara ya kwanza tangu kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa ECOWAS na kukutana na Rais Assimi Goita, ambapo kwa mujibu wa watu wa karibu na viongozi hao, ziara hiyo ililenga kuimarisha uhusiano kati ya Bamako na Dakar.
Wapiganaji kutoka katika kundi la Tuareg na wale wa JNIM wanaohusishwa na Al-Qaeda, katika miezi ya hivi karibuni wamekuwa wakitekeleza mashambulio dhidi ya utawala wa Mali, na ambapo mwezi Aprili waliuteka mji wa kimkakati wa Kidal, Waziri wa ulinzi wa Mali Sadio Camara akiuuawa katika mashambulio hayo.
Aidha nchi za Mali, Niger na Burkina Faso, zilitangaza kujiondoa katika muungano wa ECOWAS mwezi Januari mwaka wa 2025 na kuanzisha muungano wao mpya wa AES.
Tangu kuchukua madaraka kupitia mapinduzi, utawala wa kijeshi wa Mali uliahidi kupambana na makundi yenye silaha na kurejesha usalama lakini imeonekana kukabiliwa na changamoto kutoka kwa makundi hayo.





