pmbet

Senegal kunachemka Rais amtimua kazi Waziri Mkuu

Eric Buyanza

May 23, 2026
Share :

Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye amemfuta kazi Waziri wake Mkuu, Ousmane Sonko, jioni ya Mei 22, 2026. Tangazo hilo lilitolewa kwenye kituo cha televisheni cha RTS muda mfupi kabla ya saa 6:00 usiku saa za Afrika ya Kati.

 

Katika hotuba fupi iliyorushwa na shirika la Utangazaji la Senegal (RTS) kutoka Ikulu ya rais huko Dakar, Oumar Samba Ba, Katibu Mkuu katika ofisi ya rais, alitangaza kwamba Ousmane Sonko si Waziri Mkuu tena wa Senegal.

Kufukuzwa kwa Ousmane Sonko kulikuja saa chache tu baada ya kuonekana kwake mbele ya Bunge la nchi hoyo, ambapo alikuwa akijibu maswali kutoka kwa wabunge. 

"Mimi si Waziri Mkuu ambaye hukubaliana na kitu bila kuhoji," Waziri Mkuu huyo wa zamani alisema wakati wa kikao cha bunge. Katika kikao hicho pia alikiri kutokubaliana na rais kwenye baadhi ya mambo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet