pmbet

Seneta wa Nairobi aitaka Tanzania iiombe radhi Kenya

Sisti Herman

June 4, 2025
Share :

 

Edwin Sifuna, Seneta wa Nairobi na Katibu Mkuu wa Chama cha Orange Democratic Movement (ODM), ametoa wito kwa Rais wa Kenya William Ruto kuondoa kile alichokiita "msamaha feki" alioutoa kwa Tanzania, akisisitiza kuwa badala yake ni Tanzania ndiyo inayopaswa kuomba radhi kwa Kenya.

Kupitia ukurasa wake wa X, Sifuna amemtaka Rais Ruto kutekeleza mambo yafuatayo:

Kwanza kuzuia wanachama wote wa CCM kuingia nchini Kenya.

Pili, Kenya ijitoe katika maandalizi ya pamoja ya kuandaa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), ambayo yanapangwa kufanyika kwa ushirikiano na Tanzania na Uganda, kwa madai kwamba, nchi hizo mbili zinaongozwa kwa misingi ya kidikteta.

Na mwishoni, ameitaka Jumuiya ya Wanasheria wa Afrika Mashariki (EALS), kuhamisha sehemu nyengine mkutano wake wa mwaka uliopangwa kufanyika Zanzibar.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet