Sensema ya Chui na Tembo yatikisa Youtube.
Joyce Shedrack
June 15, 2024
Share :
Ikiwa ni siku moja tu tangu kuachiwa kwa ngoma mpya ya Rayvanny aliyomshirikisha Harmonize tayari imeingia kwenye rekodi ya kolabo za wasanii wa bongofleva zilizofanya vizuri ikiwa imetimiza jumla ya watazamaji milioni moja na kuwa namba moja trending huko YouTube.
Harmonize anakuwa msanii aliyehusika kwenye kolabo nyingi zilizofanya vizuri kwa mwaka huu wa 2024 mpaka kufikia mwezi huu,miongoni mwa kolabo hizo ni DHARAU aliyoshirikishwa na Ibraah pamoja na AWAY aliyoshirikishwa na Marioo.
Sensema inakuwa ngoma ya kwanza kuwakutanisha wasanii hao baada ya kupita zaidi ya miaka 5 walipokutana studio kuipika ngoma ya PARANAWE.
Unadhani msanii gani anaweza kumzidi tembo @harmonize_tz kwa kufanya kolabo kali au abatizwe mfalme wa kolabo ?.