Serena Williams kurejea kwenye Tenisi.
Joyce Shedrack
February 10, 2026
Share :
Mcheza tenisi wa Marekani Serena Williams ametangazwa kuwa anastahili kurejea kwenye tenisi ya kulipwa kuanzia tarehe 22 Februari na shirika la kupima dawa za kuongeza nguvu la mchezo huo, Wakala wa Kimataifa wa Uadilifu wa Tenisi (ITIA).:max_bytes(150000):strip_icc():focal(959x37:961x39)/Serena-Williams-Wins-First-Singles-Match-in-Over-a-year-at-Canadian-Open-080922-2-507f311fc6c24d3c94aa47f409419d20.jpg)
Hata hivyo, bado haijafahamika iwapo bingwa huyo mara 23 wa Grand Slam atarejea katika michezo ya wanawake. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 44 ziliibuka tetesi za kurejea tena mwishoni mwa mwaka jana lakini mwenyewe alikanusha.
Williams, ambaye taji lake la mwisho la Grand Slam lilikuwa mwaka 2017, hajashiriki mashindano yoyote, tangu US Open 2022.





