Serengeti Boys kupimana nguvu na Cameroon leo kuelekea AFCON U17
Sisti Herman
May 5, 2026
Share :

Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya Umri wa miaka 17 'Serengeti Boys' leo saa moja usiku itacheza mechi ya kwanza ya kirafiki dhidi ya Cameroon katika uwanja wa Mohammed V Casablanca, Morocco.
Timu ya Serengeti Boys ipo nchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya Fainali za Vijana za AFCON 2026 zinazofanyika chini Morocco 🇲🇦 Fainali hizo zitaanza Mei 13,2026 mpaka June 2, 2026.
Timu ya Vijana ya Tanzania imepangwa kundi C pamoja na nchi za Mozambique, Angola na Mali.
Timu nane zitakazofuzu kucheza hatua ya Robo Fainali na Best Loosers wawili zitakuwa zimefanikiwa kucheza Fainali za U17 Kombe la Dunia 2026 nchini Qatar.





