pmbet

Serengeti boys kuweka kambi Uingereza maandalizi ya Kombe la Dunia.

Joyce Shedrack

September 5, 2026
Share :

Msemaji wa Timu za Taifa, Haji Manara, amesema timu ya vijana ya Tanzania inatarajiwa kuelekea nchini Uingereza katikati ya mwezi huu kwa ajili ya kuweka kambi na kucheza michezo ya maandalizi kabla ya safari ya kuelekea Qatar.
Tanzania's Serengeti Boys qualify for first-ever FIFA U-17 World Cup after  3-0 win over Angola | The Eastleigh Voice
Manara amesema maandalizi hayo ni sehemu ya mikakati ya kuiandaa timu hiyo kwa ushindani mkubwa wa kimataifa, huku akiwataka Watanzania kuendelea kuwaunga mkono vijana hao pamoja na timu zote za Taifa.

Amesema sapoti kutoka kwa Watanzania ni muhimu katika kuwajenga wachezaji kisaikolojia na kuwapa hamasa zaidi wanapoiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa.

"Ni muhimu Watanzania kuendelea kuiunga mkono timu yetu ya Taifa. Hawa ni vijana wanaokwenda kuiwakilisha Tanzania, hivyo wanahitaji sapoti yetu na dua zetu katika safari yao," amesema Manara.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet