Serengeti yawafuata Zambia kombe la dunia
Sisti Herman
January 31, 2024
Share :
Kikosi cha Timu ya Taifa ya wanawake Serengeti Girls kimeondoka leo kuelekea Zambia kwa mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Zambia utakaochzwa Februari 3, 2024.
Serengeti ina kumbukumbu bora kwenye michuano hiyo kwani msimu jana kwa mara ya kwanza ilifuzu, ikiwa timu pekee kutoka Afrika mashariki, ikiungana na Nigeria na Morocco kuwakilisha bara la Afrika kisha ikafanikiwa kufika robo fainali ya kombe la dunia.