pmbet

Serikali ya kijeshi Mali, yatangaza kuruhusu shughuli za kisiasa kuendelea

Eric Buyanza

July 11, 2024
Share :

Serikali ya kijeshi ya Mali imetangaza kuruhusu vyama na shughuli za kisiasa kuendelea ikiwa ni baada ya kusitishwa mwezi Aprili.

“Serikali imeamua kuondoa marufuku ya vyama vya siasa na shughuli zake,” imesema taarifa ya baraza la mawaziri ambalo linatawaliwa na viongozi wa kijeshi waliochukua madaraka katika mapinduzi ya mwaka 2020.

Mkuu wa serikali ya kijeshi, Kanali Assimi Goita, alihalalisha kusimamishwa kile alichokiita upotoshaji wa vyama vya siasa, ambao ulikuwa hatari kwa mazungumzo yanayoendelea ya kitaifa kuhusu mustakabali wa kisiasa wa Mali.

Vyama hivyo wakati huo vilikuwa vinapinga uamuzi wa kanali wa kubaki madarakani kwa zaidi ya Machi 2024 na kutaka kurejea utawala wa kiraia.

Vyama vya upinzani vilisusia mazungumzo ambayo yaliendelea na wafuasi wa serikali, ambao Mei walitoa mapendekezo kuwa wanajeshi hao kuendelea kubaki madarakani kwa miaka miwili hadi mitano ya ziada, na kiongozi wa sasa aruhusiwe kushiriki uchaguzi wowote ujao wa urais.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet