pmbet

Serikali yaanza usambazaji wa kadi za kliniki za wajawazito na watoto nchini

Eric Buyanza

June 22, 2024
Share :

Serikali imeanza kusambaza vitabu vya kliniki vya wajawazito na watoto nchini ambavyo vitasambazwa katika mikoa 26 nchi nzima.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa huduma za Mama na mtoto wizara ya afya Dkt. Ahmad Makuwani Leo Juni 21, 2024 Katika Hospitali ya Taifa ya Afya ya akili Mirembe wakati wa uzinduzi wa kadi za ufuatiliaji wa afya ya mama na mtoto katika mikoa yote nchini.

“Leo hii tumeanza kusambaza kadi za afya ya mama na mtoto na kadi za wajawazito. Kadi hizi zinatosheleza kwa muda wa miezi mitatu kwa kuanzia wakati Serikali inaendelea kutengeneza kadi zingine ili kuhakikisha upatikanaji wa kadi unakuwa rahisi,” Amesema Dkt. Makuwani.

Aidha, Dkt. Makuwani amesema jumla ya vitabu milioni moja na laki mbili (1,200,000) zitasambazwa kwenye mikoa yote 26 nchini na kuhakikisha zinafikia walengwa ambapo 600,000 ni kadi za akina mama wajawazito na kadi 600,000 za watoto. 

“Lengo ni kuhakikisha kwamba taarifa muhimu za mama wakati wa ujauzito zinachukuliwa vizuri na pia kiasi kwamba mtoa huduma anamueleza kabisa nini anaweza kufanya kuhakikisha huduma ya afya ya mama na mtoto inakuwa salama”. Dkt. Makuwani ameongeza.

Aidha, Dkt. Makuwani amesisitiza kuwa kadi hizi zimenunuliwa kupitia uwekezaji mkubwa wa Serikali ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan na ahadi hiyo ilitolewa Bungeni na Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu, wakati wa uwasilishaji wa Bajeti ya Wizara ya Afya kwamba serikali itahakikisha wakina mama na watoto walio chini ya miaka mitano wanapata kadi zao na hawazilipii.

Dkt. Makuani amevionya vituo vya afya katika Halmashauri zote nchini kutowauzia wajawazito vitabu vya kliniki huku akiwataka wahudumu wa afya kusimamia vyema ugawaji wa vitabu vya kliniki ili kuwafikia walengwa.

“Wakina mama wamekuwa wakiacha kwenda kliniki kwa kuwa walikuwa wanauziwa kadi hizi. Sasa Serikali imechapisha kadi za kutosha na tutaendelea kufanya hivyo kila mwaka ili kumuepusha mama na kadhia hii”. Amesema Dkt. Makuwani. 

Na WAF – Dodoma

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet