Serikali yaonya watoto kubebeshwa rundo la madaftari
Eric Buyanza
February 26, 2024
Share :
Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe, amewataka walimu wa madarasa ya awali kufundisha kwa kufuata mtaala na siyo kuwabebesha mzigo wa begi la madaftari watoto utakaowaletea athari za kiafya katika ukuaji wao.
Hayo yamesemwa jana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. James Mdoe, wakati akifungua mafunzo kwa walimu wa madarasa ya awali katika Mkoa wa Dodoma ambayo yamelenga kuwapa ujuzi wa kufundisha.
“Kuna baadhi ya shule huko tunawabebesha watoto mzigo mkubwa kuliko umri wao, unakuta mtoto wa chekechea amebeba begi la madaftari 10 au 15 mpaka kibyongo, halafu anajazwa material (ujuzi) kibao unamfundisha mtoto wa awali hadi vitu vya darasa la saba.”
Amesema walimu walioandaliwa vizuri na vinara wa elimu ya awali hawawezi kufanya hivyo na kuwataka kuzingatia mtaala na wasiwabebeshe mzigo wa begi watoto.