Seti ya waamuzi wa Tanzania yateuliwa CAF kuchezesha mechi za kufuzu AFCON 2027
Sisti Herman
November 5, 2026
Share :

Seti ya waamuzi wa kimataifa wa Tanzania wakiongozwa na Ahmed Arajiga, Hamdan Ally, Ally Ramadhani na Nasir Salum wameteuliwa na shirikisho la soka Afrika (CAF) kuchezesha mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2027 inayozikutanisha timu za taifa za Equtorial Guinea dhidi ya Zimbabwe utakaochezwa Yaoundè Omnisports Ahm Novemba 12, 2026.





