Shabiki amjengea sanamu Tekashi
Sisti Herman
January 3, 2024
Share :
Shabiki wa muziki kutoka nchini Cuba ameonyesha mapenzi yake kwa rapa 6ix9ine kwa kumjengea sanamu na kuisimika katika moja ya mitaa nchini Cuba.
Mbunifu na mtengenezaji wa sanamu hilo Genis Osoria Vargas alichapisha picha na video za sanamu hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akiweka wazi kuwa sanamu ya 6ix9ine ililipiwa pesa taslimu na shabiki ambaye alitaka sanamu hiyo iwekwe nje ya nyumba yake ili kila atakayepita aione.
Msanii gani bongo ungetamani ajengewe sanamu?