Shabiki Ghana amvamia kocha wa timu ya Taifa baada ya kichapo Afcon
Sisti Herman
January 15, 2024
Share :
Shabiki mmoja wa timu ya Taifa ya Ghana anashikiliwa na vyombo vya ulinzi nchini Ivory Coast mara baada ya kumvamia kocha wa timu ya Taifa Ghana Chris Hughton kisa matokeo mabaya baada ya timu hiyo kuchezea kichapo cha 2-1 kutoka kwa Cape Verde jana.
Shabiki huyo inadaiwa alimvamia kocha huyo hotelini jijini Abidjan ilipo kambi ya timu hiyo ya Taifa lakini kwa bahati nzuri wanadiplomasia waliokuwepo wakamuookoa kocha.
Baada ya matokeo ya mchezo wa jana, Ghana sasa inaburuza mkia wa kundi B ambalo linaongozwa na Cape Verde wenye alama 6 huku wakifuatiwa na Misri na Msumbiji ambao waligawana alama baada ya sare ya 2-2.