pmbet

Shaffih Dauda afunguka Kelvin John kutoitwa Stars

Sisti Herman

January 3, 2024
Share :

Mchambuzi wa michezo na mwanahabari maarufu nchini Shaffih Dauda ambaye pia hujihusisha na masuala ya biashara za kuwasimamia wachezaji kupitia Shadaka Sports Management amefunguka kwa uzoefu wake mambo mbalimbali kuhusiana na sakata la kuachwa kwa wachezaji Kelvin John na Clement Mzize kwenye kikosi cha timu ya Taifa kinachoenda kushiriki AFCON kilichoitwa na kocha Adel Amrouche huku wengi wakihusisha mahausiaono binafsi kati yao na kocha kuwa mabaya kuwa sababu ya kuachwa kwao.

 

“Mimi nitazungumzia sehemu mbili, mwalimu aliweka wazi kuwa ana matatizo ya kinidhamu (kelvin) na akijirekebisha atamrudisha kwenye timu, kwa upande wa nidhamu ameshaomba msamaha kwa mamlaka zote benchi la ufundi, timu na viongozi wa shirikisho na ameshasamehewa, Changamoto kwasasa ni kiwango chake, hajacheza timu ya kwanza ya Genk ndio maana kocha hajamjumuisha kwenye kikosi hii ndiyo sababu”

 

“Lakini pia nimeona nyingine ni madai kwa mwalimu kutokumchukua Kelvin na Mzize watu wakimhusisha na uwakala, kuna mambo mengi sana hasa kwa nchi kama hizi za kwetu, tunajitoaga akili, tunajisahau kama sisi bado ni wachanga, makocha wa timu za Taifa kwenye nchi zinazoendelea kama Tanzania, Kenya huja sio tu kufundisha tunahitaji pia watumie mitandao na uzoefu wao kusaidia kuwatangaza wachezaji kwingineko na sisi kama nchi lazima tukubali kuwa hatuna mifumo ya kuwatoa nje wachezaji wetu kwahiyo anapokuja mwalimu kama Amrouche na kutumia mitandao yake kuwatoa wachezaji ili timu ya Taifa iwe bora mimi nitatofautiana na wale wanaosema anafanya biashara, biashara siyo rahisi hivyo” alimaliza Dauda kwenye video iliyochapishwa kwenye ukurasa wake wa Mtanzao wa kijamii.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet