Shalulile aitwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Namibia.
Joyce Shedrack
September 3, 2026
Share :
Mshambuliaji wa Yanga Peter Shalulile ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Namibia kitakachoshiriki mechi za kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) 2027.

Shalulile ambaye alijiunga na Yanga msimu huu akitokea Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ni miongoni mwa wachezaji 29 walioitwa na kocha mkuu Collin Benjamin katika kikosi hicho.





