pmbet

Shambulio la Israel lamuua Kamanda Mkuu wa Hezbollah

Eric Buyanza

July 4, 2024
Share :

Shambulizi la Israel limemuua kamanda wa ngazi ya juu wa wanamgambo wa Hezbollah, kusini mwa Lebanon, wakati mivutano kati ya pande hizo mbili ikiendelea kuongezeka. 

VOA imeripoti kuwa shambulio hilo la anga karibu na mji wa pwani wa Tyre limetokea wakati kuna ongezeko la juhudi za kimataifa za kidiplomasia, kuzuia mgogoro kati ya Hezbollah na jeshi la Israel kuongezeka na kuwa vita ambavyo vinaweza kusababisha mgogoro wa moja kwa moja kati ya Israel na Iran. 

Taarifa ya Hezbollah imemtaja kamanda aliyeuawa kuwa Mohammad Nimah Nasser, anayejulikana kwa jina Abu Naameh. Naameh ni afisa wa juu sana wa kundi hilo linaloungwa mkono na Iran, kuuawa tangu kifo cha Taleb Sami Abdullah, aliyeuawa katika shambulizi la anga la Juni 11. 

Kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah, amemtaja Abdullah kuwa mtu muhimu katika kundi hilo tangu mapambano yalipoanza Oktoba 8, akiongoza kikundi cha Nasr.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet