Shambulizi la droni laua watu 32 Darfur Kaskazini
Eric Buyanza
April 10, 2026
Share :

Shambulio la ndege zisizo na rubani kwenye mji wa Kutum unaodhibitiwa na wanajeshi katika jimbo la Darfur Kaskazini mwa Sudan limewaua raia wasiopungua 32, wakiwemo wanawake na watoto.
Kwa mujibu wa AFP shambulio hilo lilipiga kitongoji cha Al-Salama ambapo miili 12 ilifikishwa hospitali nusu yao ikiwa ni ya watoto, wakiwemo wanafunzi watatu wa kike.
Wengine kumi na sita walijeruhiwa, wakiwemo wanawake na watoto, na wanapokea matibabu, chanzo hicho kiliongeza.
Jeshi bado halijaongea chochote kuhusu shambulio hilo. Wakati huo huo vikosi vya RSF, vililaani katika taarifa yake na kuweka idadi ya vifo kuwa si chini ya 56, wakiwemo watoto 17.





