pmbet

Shangwe la mdogo wake Lamine Yamal kweye bao la Oyarzabal lazua gumzo.

Joyce Shedrack

July 3, 2026
Share :

Mdogo wa nyota wa Hispania, Lamine Yamal, anayefahamika kwa jina la Keyne, amegusa hisia za mashabiki wa soka duniani baada ya kunaswa akishangilia kwa furaha kubwa bao la Mikel Oyarzabal katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Austria kwenye Kombe la Dunia 2026.

 

Baada ya Oyarzabal kufunga bao la tatu la Hispania, kamera zilimuonyesha Keyne akiwa ameruka kwa furaha, akipunga mikono na kupaza sauti kwa shangwe, tukio lililosambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii na kuwavutia mashabiki pamoja na wanasoka wengi.

Lamine Yamal's adorable three-year-old brother goes viral for passionately  cheering Spain star on at World Cup

Akizungumzia video hiyo iliyosambaa, Lamine Yamal alisema mdogo wake ana nafasi ya kipekee moyoni mwake na kwamba humchukulia "kama mwanangu," akionyesha jinsi walivyo karibu. 

 

Shangwe za Keyne zimekuwa miongoni mwa matukio yaliyovutia zaidi nje ya uwanja katika Kombe la Dunia 2026, zikionyesha jinsi soka linavyoweza kuunganisha familia na kugusa hisia za watu duniani kote.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet