pmbet

Shaw aumia tena mazoezini United

Sisti Herman

December 4, 2024
Share :

Ikiwa ni siku kadhaa tangu arejee kutoka kwenye majeraha yaliyomuweka nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi mitatu, beki wa klabu ya Manchester United na timu ya Taifa ya Uingereza Luke Shaw ametangaza tena kupata majeraha mapya mazoezini ambayo yatamuweka nje wa Uwanja kwa kitambo kidogo.

"Najua kuna watu watakuwa wamekereka kwasababu ya hali hii lakini niwaambie hakuna mtu aliyeumizwa zaidi na jambo hili zaidi yangu, naahidi kurejea nikiwa bora zaidi" alisema Shaw kwenye sehemu ya ujumbe aliochapisha mtandao wa Instagram.

Baada ya kurejea Shaw wamecheza mechi 3 zikizopita za United ikiwemo 2 za ligi kuu Uingereza na Moja ya kombe la Ligi ya Europa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet