Shearer aishauri Newcastle kumsajili De Gea
Eric Buyanza
December 27, 2023
Share :
Mchezaji wa zamani wa Newcastle United, Alan Shearer ameitaka klabu yake hiyo ya zamani kumsajili kipa wa zamani wa Manchester United David de Gea katika dirisha la usajili la Januari.
Newcastle ilipoteza 3-1 jana dhidi ya Nottingham Forest ikiwa nyumbani.
Matokeo hayo yanawafanya wabaki pointi saba nyuma ya Tottenham Hotspur walio katika nafasi ya nne ambao wamecheza mechi pungufu.
Meneja wa Newcastle Eddie Howe anakabiliwa na majeruhi wengi kwenye kikosi chake msimu huu, akiwemo mlinda mlango Nick Pope ambaye yuko nje kwa miezi minne baada ya kuteguka bega.