pmbet

Sherehe za EURO 2024 zawatia matatani Rodri na Morata.

Joyce Shedrack

July 21, 2024
Share :

Wachezaji nyota wa Timu ya Taifa ya Hispania Rodrigo Cascante (Rodri) ambaye ni mchezaji bora wa mashindano ya EURO 2024 na Nahodha Alvaro Morata huwenda wakakumbana na adhabu ya kufungiwa mechi mbili kutokana na kosa la utovu wa Nidhamu wakati wa sherehe za ubingwa wa EURO 2024 zilizofanywa na Timu ya Taifa hilo jijini Madrid.

Shirikisho la Mpira wa Mguu Ulaya (Uefa) limefungua jalada la uchunguzi juu ya wachezaji hao kutokana na kitendo walichofanya wakati wa sherehe za ubingwa wa Euro 2024 waliochukua nchini Ujerumani baada ya kuifunga Timu ya Taifa ya Uingereza mabao 2-1.

Katika sherehe za ubingwa huo zilizofanywa katika Jiji la Madrid siku ya Jumatatu Morata alianzisha wimbo uliokuwa ukiimba hivi: “Ni Hispania Gibraltar ni Hispania pia”, akimaanisha eneo dogo lililopo kusini mwa Hispania ambalo linamilikiwa na Uingereza kuwa ni mali ya Hispania.

Baada ya Morata kuimba hivyo kiungo wa kati wa Manchester City Rodri alichukua kipaza sauti na kuendeleza wimbo huo ulioitikiwa na mashabiki waliokuwepo.
 

Gibraltar linatambulika kama eneo linalomilikiwa na Uingereza japo mara kadhaa Hispania ilijaribu kutaka kulifanya kuwa sehemu ya nchi hiyo jitihada ambazo mara zote zimekuwa zikishindikana.
 

Shirikisho la soka la Gibraltar liliwasilisha malalamiko kwa Uefa mapema wiki hii na tayari Mamlaka hiyo ya mpira Duniani Uefa imemteua mtu kwa ya kuchunguza na kama wakikutwa na hatia hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya wachezaji hao.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet