Shida nyingine Man United, Klabu tatu zamgombea Mejbri!
Eric Buyanza
December 28, 2023
Share :
Kupitia account yake ya X leo hii, mwandishi bora wa habari za michezo duniani, Fabrizio Romano amethibitisha kuwa kuna klabu tatu zinazotaka kumsajili kiungo wa kati wa Manchester United Hannibal Mejbri katika dirisha la uhamisho la Januari.
Romano pia ameweka wazi kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Tunisia hatarudi nyumbani kushiriki Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) Januari 2024.
"Hannibal Mejbri, hatakwenda AFCON kwani anaweza kuondoka Man Utd kwenda kwa mkopo Januari," Romano alitweet.
"Fahamu vilabu 3 [Sevilla, Olympique Lyon na Freiburg] wanataka kumsajili - zote zinamtaka apatikane Januari/Feb.......Wakati huo huo, mazungumzo ya kuongeza mkataba wake wa Man United yanaendelea." alimalizia Fabrizio.