pmbet

Shida ya Umeme Bongo sasa basi, Bwawa la Nyerere kuwashwa Januari

Eric Buyanza

December 18, 2023
Share :

Serikali inatarajia kuwasha kinu cha kwanza cha kufua umeme mwezi Januari, 2024 katika Bwawa la Nyerere (JNHPP) ikiwa ni jitihada za kuzalisha umeme wa kutosha.

Hayo yalisemwa na Rais Samia mwishoni mwa wiki, wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za Rais kwa wazalishaji bora (President’s Manufacturer of the year Awards – PMAYA) iliyofanyika Dar es salaam. 

“Pamoja na jitihada nyingine za gesi, sola na mambo mengine, lakini katika umeme wa maji, tunategemea nadhani katikati ya mwakani malalamiko mengi yatakuwa yamepungua,” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia amesema uwashwaji wa kinu cha kwanza utafuatiwa na uwashwaji wa kinu cha pili mnamo Aprili, 2024 lengo ni kuhakikisha umeme nchini unakuwa wa uhakika.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet