pmbet

Shilingi Bilioni 4 kujenga hospitali ya rufaa Ukerewe

Eric Buyanza

March 15, 2024
Share :

Shilingi Bilioni 4/= zimetengwa kwenye bajeti ya mwaka huu, 2023/24 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Ukerewe, mkoani Mwanza ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za Afya ikiwemo huduma za Kibingwa, katika kisiwa hicho.
 

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu, akiwa kwenye ziara mkoani Mwanza, ambapo aliambatana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI, chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Stanslaus Nyongo.
 

Amesema, fedha hizo zimepelekwa mkoani ili watangaze tenda ya kupata mshauri na mkandarasi wa atakaejenga Hospitali hiyo, ili watu wa Ukerewe wapate huduma zote za Afya karibu, zikiwemo za Kibingwa. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet