Shilole na mpenzi wake waachana rasmi
Sisti Herman
May 28, 2024
Share :
Msanii wa filamu na mjasiriamali Zuwena Mohammed "Shilole" ameachana na aliyekuwa mpenzi wake Rommy 3d ambaye ni mpiga picha maarufu.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa instagram Rommy amethibitisha kuvunjika kwa penzi hilo hukua akiandika;
"Habari.....Ndugu zangu kama ambavyo mmeona kwenye mitandao na hiyo ndio hali halisi basi Mimi na aliyekuwa mwenzangu Zuwena Mohamed(Shilole)Naona tumefikia Mwisho na si Vibaya nikakubali matokeo na kumpisha Kijana mwenzangu aendeleze gurudumu hili, na Maisha yaendelee... nipende kutoa shukrani zangu za dhati kwa vile tulivyoishi siku zote za mapenzi yetu , Wabillah Tawfiq"
Je unadhani kwanini ndoa za wasanii maarufu nyingi hazidumu