pmbet

Shime aponda uwanja waliouchezea Kenya

Sisti Herman

February 8, 2026
Share :

 

Baada ya kupoteza kwa 1-0 dhidi ya Kenya, kocha wa timu ya taifa ya Tanzania ya wanawake chini miaka 20, Bakari Shime amesema wazi kuwa tatizo lilifanya wapoteze ugenini ni "uwanja mbovu," waliouchezea.

“Timu yangu haikucheza katika kiwango chake kwa sababu uwanja ni mbovu. Kenya sio kwamba hamna viwanja vizuri, ila mmefanya kusudi.

Lakini yote kwa yote, mechi haijamalizika, sasa tunakwenda kwenye pitch nzuri ya Chamazi (Azam Sports Complex, Dar es Salaam), kila mmoja anaifahamu.

Goli moja kwa sufuri kwa timu ambayo tumecheza nayo (Kenya) ni dogo sana. Tutalirudisha na tutapata matokeo mazuri."

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet