pmbet

Shirikisho lamgomea Samuel Etoo kujiuzulu

Joyce Shedrack

February 6, 2024
Share :

Kamati Utendaji ya Shirikisho la soka nchini Cameroon, imetupilia mbali barua ya kujiuzulu ya Rais wa Shirikisho hilo Samuel Eto’o.

Ombi la Samuel Eto’o kujiuzulu kama Rais wa FECAFOOT limekataliwa na kamati Utendaji bila kujali mwenendo mbaya wa timu ya Taifa ya Cameroon nchini Ivory Coast.

 

Kamati hiyo bado inaamini kuwa Eto’o ndiye mtu sahihi wa kuliongoza Shirikisho hilo.

 

Eto’o alitaka kuachia kiti hicho cha Rais wa Shirikisho la Soka Cameroon FECAFOOT sababu ikitajwa kuwa ni kufuatia kuondoshwa  kwa timu ya Taifa ya Cameroon kwenye michuano ya Mataifa Huru ya Afrika AFCON 2023 yanayoendelea Nchini Ivory Coast.

 

Timu ya Taifa ya Cameroon ilishindwa kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo baada ya kukubali kichapo cha goli mbili kwa sifuri dhidi ya Timu ya Taifa ya Nigeria.

 

Samuel Eto’o  anashutumiwa katika upangaji wa matokea na vitisho kwa wachezaji wa timu ya taifa ya Cameroon.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet