pmbet

Show ya Rayvanny yajaza uwanja Ulaya

Sisti Herman

June 28, 2024
Share :

Usiku wa kuamkia leo Juni 28, mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini Rayvanny alifanya show katika uwanja wa mpira wa ‘Air Albania Stadium’ na kupokelewa kwa shangwe na mashabiki wakati alipokuwa akipanda jukwaani.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Rayvanny amechapisha video akionesha jinsi alivyopokelewa kwa shangwe na mashabiki kwa kumuwashia tochi huku akiweka wazi kuwa uwanja huo ulikuwa ‘sold out’ ambapo unakadiriwa kuingiza zaidi ya watu 20,000.

Rayvanny alitangaza kufanya show Albania mapema wiki ambapo alitaka kuwafunga midomo wadau wote waliyokuwa wakidai kuwa wasanii wa Bongo wakienda kutumbuiza nchi za watu huwa wanafanya show sebuleni.

Hii sio mara ya kwanza kwa Chui kupokelewa vizuri na mashabiki utakumbuka kuwa mwaka 2022 alipokelewa kwa shangwe jijini Paris wakati alipokuwa akitumbuiza na msanii kutoka Columbia, Maluma.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet