pmbet

Show ya Shakira Nchini Qatar yapigwa chini kisa vita ya Iran.

Joyce Shedrack

March 24, 2026
Share :

Tamasha la Shakira, lililokuwa lifanyike Doha, Qatar Aprili 1 kama sehemu ya ziara yake ya dunia, limeahirishwa kutokana na kile kilichoelezwa kuwa “hali ya kikanda.”.
Shakira | Songs, Age, Waka Waka, Biography, Full Name, & Facts | Britannica
Wakati huo huo, waandaaji wa Tamasha la Muziki la OFFLIMITS mjini Abu Dhabi lililokuwa lifanyike Aprili 4, likiwashirikisha Shakira pamoja na kundi la Jonas Brothers nalo pia limeahirishwa hadi Novemba.

Athari hizo pia zimegusa wasanii wengine, ambapo mwimbaji Josh Groban amefuta maonesho yake yaliyokuwa yafanyike Dubai na Bahrain katika siku zijazo kutokana na hali ya mvutano wa kikanda.

Hatua hizi zinaonyesha athari za moja kwa moja za mvutano wa kikanda katika shughuli za burudani na michezo katika eneo la Ghuba.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet