pmbet

Shughuli za vyama vya siasa zapigwa 'Stop' nchini Mali

Eric Buyanza

May 14, 2025
Share :

Serikali ya kijeshi nchini Mali imetangaza kusitisha shughuli zote za vyama vya siasa nchini humo. 

Waziri anayehusika na mageuzi ya serikali, Mamani Nassire, ametangaza uamuzi huo kupitia taarifa iliyotolewa kwenye televisheni ya taifa.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limeukosoa uamuzi huo, likisema ni pigo jingine kwa demokrasia nchini Mali.

Itakumbukwa mnamo mwezi Aprili, mawaziri walipendekeza muda wa kiongozi wa kijeshi Assimi Goita uongezwe hadi mwaka 2030.

Goita ambaye aliingia madarakani kupitia mapinduzi, ameahidi kuandaa uchaguzi japo mipango hiyo imeahirishwa bila ya kutolewa muda maalum wa kufanyika kwa uchaguzi huo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet