Shule na maofisi kufungwa kesho jijini Mexico
Eric Buyanza
June 10, 2026
Share :
Shule zote za binafsi na za umma katika Jiji la Mexico zitafungwa kesho Alhamisi huku wafanyakazi wa serikali na sekta binafsi wakishauriwa kufanyia kazi nyumbani kuelekea mechi ya kwanza ya ufunguzi wa Kombe la Dunia.
"Agizo hili ni ili sherehe za ufunguzi zifanyike bila msongamano wa magari katika siku hiyo ya ufunguzi wa Kombe la Dunia," amesema Rais wa Mexico Claudia Sheinbaum ambaye ndiye aliyetoa amri hiyo.






