pmbet

Shule zafungwa barani ulaya kutokana na joto kali

Eric Buyanza

June 22, 2026
Share :

Mataifa ya Ulaya yanakabiliwa na wimbi la joto kali huku yakilazimika kuchukua hatua kadhaa ili kuepusha maafa, ikiwemo kufungwa kwa shule, kufutwa kwa michezo ya nje na safari za treni.

 

Hili ni wimbi la pili la joto kali kushuhudiwa eneo la Ulaya Magharibi katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja, wiki hii ikitarajiwa kuwa na viwango vya juu vya joto. Serikali ya Ufaransa imeviweka vikosi vya dharura na jeshi katika hali ya tahadhari kutokana na hatari ya kuzuka moto wa nyika huku ikipiga marufuku unywaji wa pombe hadharani.
 

Waziri Mkuu wa Ufaransa Sebastien Lecornu amesema serikali inaandaa mikakati ya muda mrefu ya kukabiliana na mawimbi ya joto kali, ikiwemo matumizi makubwa zaidi ya viyoyozi pale itakapohitajika na kwamba imeimarisha utayari wa kukabiliana na moto wa misitu, na kuagiza uangalizi mkali wa usambazaji wa maji katika mitambo ya nyuklia.
 

Mataifa ya Ufaransa, Ujerumani na Uhispania na yametangaza kufuta baadhi ya michezo iliyotarajiwa kufanyika nje, kutokana na wimbi kali la joto linaloyakumba mataifa mengi ya Ulaya , ambako katika baadhi ya maeneo kunatarajiwa hadi nyuzi joto zaidi ya 40 Celsius.

 

Nchini Ufaransa, karibu nusu ya maeneo yote imewekwa katika hali ya juu ya tahadhari kutokana na joto kali huku mamlaka zikitaja kuwa asilimia 90 ya idadi jumla ya watu nchini humo wataathiriwa na wimbi hili la joto huku hatua kadhaa zikichukuliwa kujaribu kupunguza athari hasa kwa wafanyakazi katika sekta ya ujenzi na mashuleni.

 

Jumla ya shule 845 zimefungwa leo Jumatatu, huku shule zingine zaidi ya 1,500 zikitangaza kuwa zitawaruhusu wanafunzi kuondoka mapema. Watu wanashauriwa kutokaa juani kwa muda mrefu, kunywa maji kwa wingi. Marielle Salehi ni mkazi wa Paris.
 

"Nina bahati kwamba nyumbani kwangu joto si kali sana. Kwa hivyo, leo nilitoka asubuhi tu na nikarejea nyumbani na sijatoka mchana wote huku nikiwa nimefunga mapazia. Hali ilikuwa sawa, lakini joto ni kali sana. Hasa usiku na hizi sherehe na muziki, watu wakicheza, wakinywa na kadhalika. Hakika, kuna watu wengi," alisema mkazi huyo wa Paris.
 

DW

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet