Si 'Block' wakosoaji, nataka waone navyopiga hatua - Davido
Eric Buyanza
September 17, 2025
Share :
Mkali wa muziki kutoka Nigeria, David Adeleke, maarufu kama Davido ameeleza sababu zake za kwanini hawa-block wanaomsema vibaya mitandaoni.
Kupitia akaunti yake rasmi ya X, Davido alifichua kwamba huepuka kimakusudi kuwablock wakosoaji kwa sababu anataka waendelee kuona maendeleo na mafanikio yake.
Kwa mujibu wa Davido, kama angewafungia wakosoaji wake kwenye mitandao yake ya kijamii basi kungewanyima fursa ya kushuhudia jinsi anavyopiga hatua kwenye muziki na maisha yake binafsi.