Siamini katika makasiriko maisha yanahitaji furaha - Mkojani
Eric Buyanza
April 10, 2025
Share :
Msanii wa vichekesho nchini, Mkojani amesema siyo kazi ndogo kuwafanya mashabiki kucheka kwani changamoto za kimaisha ni nyingi na siku zote yeye haamini katika makasiriko kwani maisha yanahitaji furaha.
“Kwanza ukikaa na mimi muda wote utacheka, kwani siamini katika makasiriko maisha yanahitaji furaha, na uhai ni zawadi tosha kutoka kwa Mwenyenzi Mungu.”
“Mashabiki wangu wajiandae kwa kucheka maana sina kazi mbovu, ninatoa mafunzo na kuburudisha na mwaka huu utakuwa wa mafanikio makubwa,” alisema Mkojani.
Mwanaspoti