Siasa za kisasa ni kutatua changamoto, sio maneno matupu - Simbachawene
Eric Buyanza
July 12, 2024
Share :
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene amesema siasa za kisasa ni kutatua changamoto zinazowakabili wananchi na sio kuzungumza maneno matupu huku.
Amewataka wananchi kuwapuuza wale wote wanaokejeli maendeleo yaliyofanywa na Serikali jimboni kwake na nchini kote kwa ujumla.
Simbachawene amesema hayo wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Kibakwe, Jimbo la Kibakwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma ambapo amesema Kibakwe ya sasa ni tofauti na ile ya miaka kadhaa iliyopita.
Amesema mfano mwaka 2005 jimbo hilo lilikuwa dhoofu kwenye huduma za kijamii ikiwemo elimu, afya, maji, umeme pamoja na barabara lakini kwa sasa imekuwa ni tofauti.