Sijafanikisha jambo lolote la maana kwenye tasnia ya muziki - Wizkid
Eric Buyanza
March 9, 2024
Share :
Pamoja na umaarufu alionao Afrika na duniani kwa ujumla, pamoja na kazi ambazo ameshafanya akiwashirikisha wasanii wakubwa duniani, mwanamuziki wa Nigeria Ayodeji Balogun (Wizkid) amesema safari yake kama mwanamuziki ndio kwanza inataka kuanza.
KWANINI ANASEMA HIVYO?
Kwa mujibu wa Wizkid, anasema hajapata mafanikio yoyote makubwa ya maana katika muziki mpaka sasa ambayo yamemridhisha.
Akizungumza katika mahojiano na BBC Radio 1Xtra, Wizkid alisema: “Safari inakaribia kuanza kwa Wizkid. Sijioni kama mtu ambaye amepata kitu kikubwa bado. Kwangu mimi, muziki ni kitu cha milele." alisema.
Taarifa ikufikie tu kuwa Wizkid ni miongoni mwa wasanii wanaolipwa fedha nyingi zaidi barani Afrika na ndiye msanii aliyetunukiwa tuzo nyingi zaidi Afrika.
Ni mwanamuziki wa pili wa Nigeria mwenye mashabiki wengi zaidi kwenye mitandao ya kijamii baada ya Davido