pmbet

"Sijapata usingizi kwa miaka 60, na sijaathirika kwa lolote" - Thai Ngoc

Eric Buyanza

April 12, 2024
Share :

Huko nchini Vietnam, mkulima aitwae Thai Ngoc, mwenye umri wa miaka 80 anadai kwamba hajalala kwa zaidi ya miaka 60, na kukosa usingizi hakujaathiri maisha yake kwa vyovyote.

Wengi wetu hatuwezi kuishi bila kulala angalau kwa masaa machache, lakini mzee huyu amezua gumzo kwenye vyombo mbalimbali vya habari duniani baada ya kudai kwamba ametumia miaka yake 60 iliyopita akiwa macho, bila hata kulala kwa muda mfupi. 

Familia ya Ngoc, mke, watoto pamoja na marafiki wanathibitisha kwamba hawajawahi kumuona mzee huyo akiwa amelala.

"Sijui kama kukosa kwangu usingizi kumeathiri afya yangu au la, lakini bado nina afya njema na ninaweza kufanya kazi ya shamba kama wengine," Thai Ngoc aliiambia tovuti ya Thahn Nien News.

Mzee huyu aliyezaliwa mwaka 1942, anadai kwamba alipatwa na homa kali sana akiwa na umri wa miaka 20, na tangu kipindi hicho hakuweza kulala tena...licha ya kujaribu dawa mbalimbali za kizungu, tiba asili na hata pombe kama alivyoshauriwa na baadhi ya marafiki.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet