Sijawahi hata siku moja kuwa na tabia ya kubadilisha wanaume
Eric Buyanza
July 17, 2025
Share :
Mwanamuziki na muigizaji Lulu Diva ameonyesha kukerwa na maneno aliyodai ya uzushi ambayo yamekuwa yakitolewa dhidi yake hasa kupitia mitandao ya kijamii ambapo baadhi yao wamediriki kusema anabadilisha wanaume kila uchao kitu ambacho anasema sio kweli.
“Naomba niseme kitu na nieleweke tafadhali, sijawahi hata siku moja kuwa na tabia ya kubadilisha wanaume, yaani kuwa na msururu wa wanaume kama wanavyoniorodheshea, mara naambiwa huyu mara huyu mara yule niacheni jamani nimechoka,” alisema Lulu Diva.
“Mie nimechoka na hizi taarifa, yaani kila mwanaume nahusishwa naye...ebu watu waniache. Waache kufuatilia maisha yangu na kunizushia vitu nisivyokuwa navyo, vinaniumiza sana,” alisisitiza Lulu.
“Kama watu nawakera na maisha yangu basi usiyafuatilie sio lazima, niacheni mimi nafanya kile kinachoridhisha nafsi yangu maana sipendi kujikasirisha. nakuwa nao karibu kiurafiki tu wa kawaida.”
MWANASPOTI