Sijawahi kutamka neno 'Nakupenda' kwa mtu yeyote - Falz
Eric Buyanza
July 27, 2024
Share :
Katika hali ya kushangaza Rapa wa Nigeria Falz, amedai kuwa hajawahi kuwa na upendo na mtu yeyote.
Akizungumzia maisha yake ya mapenzi katika mahojiano na Podcast ya Menisms, Rapa huyo alisema hajawahi kufikia hatua katika mahusiano ya kutamka neno 'I LOVE YOU / NAKUPENDA'.
"Sijawahi kusema NAKUPENDA kwa mtu yeyote, yaani sijawahi kuwa katika mapenzi hadi nikafikia kwenye kiwango hicho cha hisia.....sijawahi kufika huko” anasisitiza Falz.