Sikia kituko hiki cha mwizi mstaarabu zaidi duniani
Eric Buyanza
July 4, 2026
Share :

Mwaka 2022 jamaa mmoja aliyefahamika kwa jina la Marcus Renard Hubbard, alipata umaarufu mkubwa mtandaoni baada ya kufanya tukio la kushangaza na kufurahisha huko Texas nchini Marekani.
Jamaa huyu ambaye wengine walimwita "mwizi mstaarabu" alivunja nyumba ya mtu usiku ili kuiba mashine ya kukata nyasi, lakini kabla ya kuondoka nayo
Marcus aliiweka mafuta na kuanza kufyeka nyasi zote za uwanja wa nyuma kwa umakini mkubwa, na kisha akahamia uwanja wa mbele wa nyumba hiyo.
Video za usalama zilimuonyesha akifanya kazi hiyo kwa utulivu huku magari yakipita barabarani na taa zao zikiwa zinamulika.
Sauti ya mashine hiyo usiku wa manane ilimwamsha mwenye nyumba, ambaye alipochungulia nje alishangaa kuona mtu asiyemjua anamsafishia uwanja wake. Mwenye nyumba alipiga simu polisi. Polisi walipofika eneo la tukio, walimkuta Marcus akiwa anamalizia kukata nyasi za uwanja wa mbele. Alipowaona polisi, alikimbia huku akiburuta ile mashine ya nyasi.
Wakati anakimbizwa na polisi akaona isiwe tabu akaitupa mashine ile kwenye uchochoro na kufanikiwa kutoroka.





