pmbet

Siku 6 za moto za Makonda zimeanza leo

Eric Buyanza

May 23, 2024
Share :

Siku 6 za moto alizotangaza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Kufanya Mikutano ya Hadhara kwenye halmashauri sita za Mkoa wa Arusha zinatarijiwa kuanza leo katika Wilaya ya Longido.
 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Magari ya Jeshi la Zimamoto na Ukoaji Mkoani Arusha, Mhe. Makonda alisema katika mikutano ya hadhara atasikiliza na kupokea kero za wananchi wa maeneo hayo ja kuwataka Watendaji wa ngazi zote kuanzia ngazi ya Mtaa/ kitongoji, Kijiji, Kata, halmashari, Wilaya hadi Mkoa kujiandaa ipasavyo kuwa na majibu ya kero hizo na kueleza kuwa, hatovumilia uzembe, ubadhirifu ama kusuasua kwa miradi ya maendeleo kunakofanywa kwa makusudi na baadhi ya watendaji.
 

Mhe. Mkuu wa mkoa amewasisitiza wananchi wote wa mkoa wa Arsuha kuhudhuri Mikutano hiyo ya Hadhara katika halmashauri zao kwa tarehe zilizopangwa ili kuweza kuzungumza pamoja na wenye kero kuziwasilisha kupitia mikutano hiyo huki akendelea kuahidi kuwa wananchi wote walodhulumiwa haki zao atahakikisha wanarejeshewa.
 

Ziara hiyo inaanza rasmi siku ya leo katika wilayani Longido kabla ya kuelekea Halmashauri ya Karatu Mei 24, Monduli Mei 25, Mei 28 halmashauri ya Arusha, halmasahuri ya Meru Mei 29, 2024 na hitimisho la siku zake sita litakuwa kwenye Jiji la Arusha tarehe 30, Mei 2.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet