pmbet

Silaha hatari zinazotumiwa na Marekani dhidi ya Iran

Eric Buyanza

March 27, 2026
Share :

NDEGE YA KISASA YA B-2 SPIRIT

Moja ya silaha muhimu zaidi iliyotumika katika mashambulizi haya ni ndege ya kivita ya masafa marefu aina ya B-2 Spirit. Ndege hii ni miongoni mwa teknolojia za juu zaidi katika Jeshi la Anga la Marekani, ikiwa na uwezo wa kuepuka kugunduliwa na rada za adui.

 

B-2 Spirit imeundwa mahsusi kwa ajili ya mashambulizi ya kimkakati dhidi ya malengo yenye ulinzi mkali, kama vile vituo vya nyuklia na maghala ya silaha.

Katika operesheni hii, ndege hizi ziliruka kwa zaidi ya saa 30 kutoka Marekani hadi Iran, zikifanya mashambulizi ya moja kwa moja dhidi ya malengo muhimu. Uwezo wake wa kuruka umbali mrefu bila kujaza mafuta unaiwezesha kufikia karibu eneo lolote duniani.
 

Ndege hii inaweza kubeba mabomu mazito, ikiwemo yale ya kuvunja ngome (bunker busters), ambayo hutumika kushambulia maeneo yaliyofichwa chini ya ardhi.

 

MAKOMBORA YA TOMAHAWK

Makombora haya ya masafa marefu ambayo hurushwa kutoka kwenye meli za kivita au manowari. Makombora haya yana uwezo wa kusafiri umbali mrefu sana na kulenga shabaha kwa usahihi mkubwa, yakitumia mifumo ya kisasa ya uongozaji (navigation systems). Katika mashambulizi dhidi ya Iran, Tomahawk zilitumika kulenga vituo muhimu vya kijeshi na miundombinu, hasa katika hatua za mwanzo za operesheni.

Faida kubwa ya makombora haya ni uwezo wake wa kurushwa kutoka mbali bila kuhatarisha maisha ya marubani, jambo linalopunguza hatari kwa vikosi vinavyoshambulia.
 

'DRONI' ZA MQ-9 REAPER

MQ-9 Reaper ni moja ya silaha muhimu katika vita vya kisasa, ikitumika kwa upelelezi na mashambulizi kwa wakati mmoja.

Ndege hii isiyo na rubani ina uwezo wa kukaa angani kwa zaidi ya saa 27, ikikusanya taarifa muhimu za kijeshi na pia kushambulia.

Katika mashambulizi dhidi ya Iran, MQ-9 ilitumika kufuatilia mienendo ya majeshi pamoja na kulenga malengo kwa usahihi mkubwa.

Ina uwezo wa kubeba makombora na silaha nyingine, jambo linaloiwezesha kufanya mashambulizi ya ghafla bila kutoa onyo.
 

BBC

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet