pmbet

Simba 10 wauawa kwa Sumu Ngorongoro

Sisti Herman

September 20, 2026
Share :

 

Simba 10 wamekufa katika eneo la Ndutu, Kata ya Endulen, Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha, huku Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) ikisema uchunguzi wa awali unaonyesha uwezekano wa wanyama hao kuuawa kwa kulishwa sumu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na NCAA leo Jumamosi, Septemba 19, 2026, tukio hilo lilitokea Septemba 18, 2026 katika eneo hilo.

Mamlaka hiyo imesema imeanza uchunguzi wa kina wa kitaalamu ili kubaini chanzo na wahusika wa tukio hilo, huku ikieleza kuwa taarifa zaidi zitatolewa baada ya uchunguzi kukamilika.

“Taarifa za awali, uchunguzi unaonyesha kuwa wanyama hao wanaweza kuwa waliuawa kwa kulishwa sumu,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

NCAA imesema uchunguzi huo unalenga kubaini chanzo cha tukio na wahusika, pamoja na kupata taarifa kamili kuhusu mazingira yaliyopelekea vifo vya simba hao.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet