pmbet

Simba haina kosa na ishu ya Selemani Mwalimu kujiunga na Yanga

Eric Buyanza

August 12, 2026
Share :

MO anazingua. Mangungu hatufai. Viongozi wetu hawana uchungu na timu. Inakoendea kuna siku tutaamka na kuona GSM ameinunua timu yetu. Haya ni maneno ya mashabiki wa Simba katika siku ya jana ambayo Yanga walitangaza kumsajili mchezaji wa Waydad Casablanca Seleman Mwalimu ‘Gomez’.

 

Kiufupi tu, katika usajili wa Mwalimu kujiunga na Yanga hakuna mwenye kosa kwenye upande wa Simba. Sio MO. Sio Mangungu wala sio Magori. Hakuna mwenye kosa la moja kwa moja.

 

Simba walikubaliana kila kitu kwa mdomo na Waydad Casablanca kuwa pesa ilipwe leo Jumatano na biashara ikafungwa hapo. Kilichotokea Waydad wamepokea ofa ya fedha nyingi zaidi ya ile waliokubaliana kwa mdomo kutoka kwa Yanga. Unadhani nini kingetokea?
 

Mwalimu amepewa tu maelekezo na alichokifanya ametekeleza kile alichoambiwa na Waydad ambayo kimsingi ndio timu yake mama. Hata Mwalimu mwenyewe hapaswi kubeba chembe yoyote ya lawama.

 

Walichokifanya Yanga kinafanyika sana katika mipira na hakuna kesi ambayo wanatakiwa kuijibu. Walichokifanya ni kitu cha kawaida kabisa. Mpira ni mchezo mchafu.

 

Mahusiano ya karibu ya Rais wa Waydad na Rais wa Yanga, ndiyo yaliyoirahisisha hii biashara. Hakuna kingine. Wanaopaswa kubeba lawama katika hili ni Waydad ambao wameshindwa kusimamia makubaliano, ambayo bado huwezi kuwalaumu sana.

 

Makubaliano yao na Simba ni ya mdomo. Hakuna sehemu ambayo unaweza kuwafunga Waydad. Nimependa alichokijibu Mangungu alipofanyiwa mahojiano na chombo kimoja cha habari jana.

 

“ Mimi nafikiri unaopaswa kuwauliza nini kimetokea katika hili ni Waydad na sio sisi Simba “

 

@abdulmkeyenge1

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet