Simba hasira zote kwa Mashujaa leo
Sisti Herman
April 9, 2024
Share :
Klabu ya Simba leo Saa 10 jioni itashuka dimba la Lake Tanganyika kumenyana na Mashujaa Fc mjini Kigoma kwenye mchezo wa raundi ya nne wa kombe la Shirikisho la CRDB.
Hiyo itakuwa mechi ya kwanza kwa Simba baada ya kuondolewa kwenye hatua ya robo fainali ya ligi ya Mabingwa Afrika na Al Ahly mwishoni mwa wiki iliyopita nchini Misri.