Simba kuajiri Mkurugenzi wa wanachama, yatangaza nafasi ya kazi
Sisti Herman
June 6, 2024
Share :
Klabu ya Simba kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii imetangaza fursa ya kuajiri nafasi ya Mkurugenzi wa Wanachama.
Akizungumza kuhusu nafasi hii Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula amesema, “Hii ni nafasi muhimu sana katika klabu yetu hivyo tunakaribisha waombaji wenye vigezo vilivyotajwa hapo juu kuleta maombi yao ndani ya muda uliopangwa. Tumedhamiria kuimarisha Idara ya Wanachama na Mashabiki ili kuwapa Wanachama wetu huduma bora, kusogea karibu yao na kuboresha uandikishaji wanachama baada ya Katiba ya Simba kuondoa ukomo wa namba ya Wanachama.”